Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Nouri al-Maliki, Mwenyekiti wa Muungano wa Dola ya Sheria wa Iraq, sambamba na kuwasili kwa mwili wa Imam Shahidi Khamenei katika Uwanja wa Ndege wa Najaf Ashraf, alisema: "Kuhifadhi urithi wa Imam Shahidi Sayyid Ali Khamenei na kushiriki katika hafla ya mazishi yake ni wajibu; kwa sababu alikuwa kiongozi mkubwa aliyesimama imara, akadumu thabiti, akakabiliana na maadui na kuuletea ushindi taifa la Iran."
Al-Maliki alisema: "Lolote ambalo taifa la Iraq linatoa kupitia ushiriki wake katika mazishi haya na misimamo mingine, japokuwa ni jambo kubwa, bado ni dogo mbele ya haki ya mtu huyu mkubwa ambaye alijenga mustakabali mkubwa si kwa taifa la Iran pekee, bali pia kwa mataifa yote ya eneo hili."
Aliongeza: "Kila tunachokifanya leo ni sehemu ya wajibu wa kuhifadhi kumbukumbu ya kiongozi huyu mkubwa ambaye alisimama imara, akadumu thabiti na akakabiliana na madola makubwa yaliyokuwa yakijulikana kwa uwezo wao mkubwa wa kijeshi. Aliweza kufanikisha ushindi, na taifa la Iran, kwa baraka za subira, ustahimilivu na uimara wake, liliibuka mshindi licha ya ukubwa wa changamoto na hasara zilizolikumba."
Aidha alisema kuwa; matokeo ya hayo yalidhihirika katika mafanikio ya Jamhuri ya Kiislamu, iwe katika uwanja wa mazungumzo ya kisiasa au katika medani za mapambano.
Nouri al-Maliki alisisitiza: "Ujumbe wa wazi wa Iraq leo unathibitisha kwamba Jamhuri ya Kiislamu haiko peke yake; ipo watu wanaosimama pamoja nayo na kuiunga mkono. Iko katika haki, na ina wafuasi wengi katika maeneo mbalimbali duniani, hata kama baadhi ya mataifa hayawezi kueleza hilo waziwazi kutokana na mazingira ya kisiasa wanayoishi ndani yake."
Maoni yako